Chapeo Ya Wokovu
@ChapeoYaWokovu
Soma Neno Ukue Kiroho
Najua unatamani kusoma biblia kila siku, Ulijaribu kufanya hivyo na ukaishia njiani, Mwaka huu ulipanga kabisa kusoma biblia kila siku na uliishia njiani. Njia rahisi ni kuwa na Nia na kukaa karibu na wenzako wanaosoma biblia kila siku. Karibu group la wasap +255759808081.

2 Mambo ya Nyakati 32:8 kwake upo mkono wa mwili; ila kwetu yupo Bwana, Mungu wetu, kutusaidia, na kutupigania mapigano yetu. Na watu wakayategemea maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.
Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi. Mt 20:26-28
Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu. 1 Sam 2:2 SUV
Zaburi 93:4 Kupita sauti ya maji mengi, maji makuu, Kupita mawimbi ya bahari yaumkayo, Bwana Aliye juu ndiye mwenye ukuu.
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Efe 6:12 SUV
Wagalatia 5:22, 23 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.
2 Wakorintho 12:9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.
Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni. [Zaburi 129:5]
Zaburi 77:1-3 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam nimpazie Mungu naye atanisikia. Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana. Mkono wangu ulinyoshwa usiku haukulegea, Nafsi yangu ilikataa kufarijika. [3]Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika, Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.
Mathayo 7:11 Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Toka mwisho wa nchi nitakulilia nikizimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda. [Zaburi 61:2]
"Lawama ya wazi ni heri, kuliko upendo uliositirika" MITHALI 27:5
Bila imani huwezi kuthubutu kufanya chochote cha maana hapa Duniani, na ukijaribu bila imani utaishia njiani. Imani inampa mtu nguvu na tumaini la kuendelea kukifanya kitu au kukiendea kitu.
Isaya 35:10 Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Mt 11:28 SUV
Utanijulisha Njia Ya Uzima; Mbele Za Uso Wako Ziko Furaha Tele; Na Katika Mkono Wako Wa Kuume Mna Mema Ya Milele. "ZABURI 16:11"
Hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki. Yakobo 3:17
Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Lk 9:23-24 SUV
Imani inakupeleka mahali unataka...youtu.be/i-nwTuRJoTQ?si…