Rehema Mwakalinga 馃嚬馃嚳
@RehemaGm
馃憼馃憸馃憲馃憱馃憶馃憯馃憳馃憴 #God first, #Born Again 馃拑馃挭, #Believer #Nyakyusa girl馃拑, #Manchester united/Yanga african馃挭. #Agribusiness #Airbnb service located Dar & Arush
Ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kuokuo na kunitafuta uso na kuziacha njia zao mbaya basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao hapa.
Marko 10:51-52 [51]Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona. [52]Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.
Isaya 43:4-5 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu na mwenye kuheshimiwa nami nimekupenda kwa hiyo nitatoa watu kwa ajili yako na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako. Usiogope maana mimi ni pamoja nawe nitaleta wazao wako toka mashariki nitakukusanya toka magharibi.
Isaya 43:2 [2]Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
Zaburi 77:1-3 Nimpazie Mungu sauti yangu, Naam nimpazie Mungu naye atanisikia. Siku ya taabu yangu nalimtafuta Bwana. Mkono wangu ulinyoshwa usiku haukulegea, Nafsi yangu ilikataa kufarijika. [3]Nilipotaka kumkumbuka Mungu nalifadhaika, Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia.
PRAYER TIME馃憞 Ufunuo wa Yohana 3:8 [8]Nayajua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, ambao hapana awezaye kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe umelitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.
Zaburi 138:7-8 [7]Nijapokwenda kati ya shida utanihuisha, Utanyosha mkono juu ya hasira ya adui zangu, Na mkono wako wa kuume utaniokoa. [8]BWANA atanitimilizia mambo yangu; Ee BWANA, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.
Kutoka 14:13-14 [13]Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele. [14]BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
Zaburi 50:5-6 [5]Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu. [6]Na mbingu zitatangaza haki yake, Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.
Zaburi 9:1-3 [1]Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote; Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu; [2]Nitafurahi na kukushangilia Wewe; Nitaliimbia jina lako, Wewe Uliye juu. [3]Kwa sababu adui zangu hurudi nyuma; Hujikwaa na kuangamia mbele zako.
Isaya 61:10 [10]Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye wala hataharibu mazao ya ardhi yenu wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba asema BWANA wa majeshi. Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema BWANA wa majeshi.
Malaki 3:10 [10]Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Isaya 55:7-8 [7]Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa. [8]Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.
Yeremia 17:9-10 [9]Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua? [10]Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.
Matendo ya Mitume 1:4-5 [4]Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; [5]ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.