πΎπππ£πππ ππππ π ππ ππππ (βΌοΈβΎοΈβ»οΈβοΈ)
@mollelgg
Leader|Pastoral Teacher||Wisdom Lover|Katibu Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Mvomero|Currently, Afisa Uchunguzi (W) Mvomero.
Nilichoandika ukiona hakikuhusu, wala hakikugusi - nakuomba usiache kurudi tena kusoma ukurasa wangu. Ujue tu kwamba hicho kisichokugusa ni portion ya mtu mwingine kwa muda huo. Naamini utakaporudi tena utakutana na cha kwako kitakachokusaidia. Mungu ni mwema kwetu sote. π
Ni vyema ukaweka picha nzuri kwenye profile yako siku moja picha hiyo itakuja kukutambulisha kwenye tukio jema au baya litakalokupata. Maisha yana surprise nyingi sana. Tujitayarishe kwa yote.
Usikubali shetani akukumbushe kumbushe makosa na madhaifu yako uliyotenda zamani. Lengo lake ni kukufifisha nguvu za kuanza upya. Kila mara shetani anapokuletea dhambi zako za zamani mwambie nilishatubu. Hazipo tena. Sasa hivi nimeanza upya. Uchana na mimi. Usinisumbue.
Made of HIS likeness and glory.. living by HIS Mightnes ... Mtanzania Mzalendo. Mali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. πΉπΏπ

"Shetani hawezi kukupitia kama haukuwa na miadi naye" - Mhe. Balozi @tonytogolani ππ»
Usimdharau mtu. Kesho haijafika ujue!
Mkubwa akikuzabua akiulizwa hujitetea kuwa anakuadabisha. Ila mdogo akijitetea wakati akizabuliwa na mkubwa huonekana hana adabu.
Ukikamua juice ya ndim hauwezi pata juice ya apple. Inamaanisha upendo hutoa upendo. Kama hujui jinsi ya kujipenda huwezi penda wengine.
Ningesema, βUpendo hauna maana yoyote usipoanzia kwako.β Unaweza kuuonesha kwa wengine na hujau-experience. Jitendee unachowatendea wengine.
Upendo hauna maana yeyote mpaka pale utakapouonesha kwa wengine.
Unaweza kufanya vitu vyote lakini usimnyanyasie mtu shida yake. Shida siyo kitu cha kudumu. Usipomnyooshea mikono yako, kuna vile Mungu atafanya tu kumsaidia hata pasipo wewe. Baraka za mtu hazizuiliwi na uchoyo wetu.
Maoni ya watu siyo lazima yawe sawa na ukweli wa mambo. Mengi ni mitazamo yao iliyobeba hisia na yale wanayokuwazia. Ukiwekeza nguvu kubwa kujijetea hakuondoi wala kupungua chochote kwenye maneno yao zaidi utazidi kujisikia vibaya kwa wao kutokubali unachojitetea nacho kwao.
Usipoamua kukabiliana na madhaifu yako, kuna watu siku zote wataendelea kunufaika na maamuzi yako.