Maybach The Wizard 💡
@shadradeen
Built from zero, Powered by passion. Words, Visuals, Emotions - All mine. This is more than content - It's a revolution.
Sinza duka linafunguliwa saa 5, kuna T shirt 4, Jinsi 3 ila ndani full AC, Wifi, Dstv, Nje imepaki ndinga ya milioni50+, wenzetu wanafanye 🤔.
Shule ya MAISHA haina mwalimu wala wanafunzi wenzako.
Ukitaka kujua mapenzi ni nini na watu wanakuwaje risk taker mwanamke akupende aisee 🙌.
Unaweza jenga maisha na mwanamke ambaye hapiki, I mean kwamba ndani kuna kila kitu mafuta, mchele, Unga, Gesi, nk. Lakini maisha yake ni kununua chips na soft drinks?
Maisha huwa hayakuumizi kwa makusudi, yanakufundisha kupitia wale uliowaamini sana kwa sababu sehemu ya ukuaji ni kuvunjwa mahali palipokua na matumaini mengi.
Picha inayokuja kichwani nikiskia mtu anaishi kimara.

1. Wengi wetu tunaishi kama tutapata nafasi ya kuanza tena… tukisahau kwamba hii ndio nafasi yenyewe. 2. Maisha si marathon wala sprint… ni saa inayoisha bila kurudi nyuma. 3. Tunaishi tukiweka kila kitu kwa 'baadaye' hadi maisha yenyewe yaanze kutuacha.
Umeajiriwa kwenye ofisi ambayo unalipwa kwa mwezi 400K. Baada ya kupokea mshahara, Rafiki ako unayefanyanae kazi ofisi moja kaomba umkopeshe 300K atarudisha baada ya one week, Je unaweza kumkopesha ingawa na yeye ana mshahara wake?
Uvumilivu wa kimya ndio silaha ya wenye malengo makubwa. Wakati wengine wanapoteza nguvu kwa sauti,wewe ujifunze kuendelea kwa utulivu na nidhamu.
Katika tamthilia ya kombolela kuna waigizaji watatu wamependezesha sana na kuipa mvuto. 3. Kuna yule dada aliekaa kwenye wheelchair 2. Kuna yule jamaa big mweusi (Kobisi) 1. Wa kwanza ni mzee kikala ametisha sana kaigiza kwa hisia sana . Inatizamwa na Rika zote kazi nzuri🔥🙌
Imetimia miaka saba sasa, Tangu nilipomtafutia kazi rafiki yangu ofisini kwetu na baada ya hapo kachonganisha mambo mpaka nikafukuzwa kazi. Hii dunia inatakiwa tuishi kìtaalamu sana .
Kuna kampuni moja inaitwa ALLIANCE AND GLOBAL iko mwanza pale ROCK CITY MALL kazi yao ni kutoa vijana wadogo mikoani na kuwatapeli pesa za kujiunga nao afu baada ya hapo wanawadanganya pesa zao zitaingizwa kwenye account zao mwisho wa siku wanapigwa kimya .
WASUKUMA ni watu wazuri sana, Leo nilikuwa SENGEREMA kuna nyumba nimeomba maji ya kunywa nikaletewa maji,viazi vitamu na uji 😋. WASUKUMA mungu awalinde sana WAZARAMO lolote liwakute 😄.
1. Maisha Yanapita Kimya Kimya, Je Unasikiliza? 2. Muda Hauombi Radhi… Unapita Tu 3. Tunaishi Tukiweka Kesho, Tukisahau Leo 4. Wakati ni Adui Anayevaa Uso wa Rafiki 5. Maisha Hayana Rasimu — Unachoandika Sasa Ndicho Kitakumbukwa
Hivi ni mimi tu king'amuzi kikiisha ndo nakumbuka kama kuna safari channel 😅.
Kuna muda unaweza kupita mitaa flani ya wahuni na wewe bila shida unawapa salamu, lakini wahuni wanakuangalia tu wanakula vitu vyao hii situation huwa inakata kinoma 😅😅.
Akili kubwa haishindani, haijibu mashambulizi, haina muda wa kubishana — ina focus ya kutengeneza mazingira ambayo kelele haziwezi kufika.
Kuna nyakati maisha hayakupi majibu, si kwa sababu hayana… bali kwa sababu bado hujawa tayari kuyaelewa.
Wengine huondoka kimya si kwa sababu hawajali, bali kwa sababu walilia sana bila kusikilizwa. Walijifunza kuwa ukimya ni kinga, na tabasamu ni hifadhi ya maumivu. Na walipoondoka bila kelele, walikuwa wamefika mwisho wa matumaini.
Kuna maumivu hayaponywi na muda. Yanabadilika tu kuwa sehemu ya akili yako ya tahadhari.