ZITATU
@max_zitatu
Mafundi wengi wa furniture, tena sana hawa vijana vijana.. Ukicheki simu zao, huwezi kuikosa pinterest..
Mwanamke wako anapaswa kuwa na tabia njema na awe mstaarabu. Kama haonyeshi thamani yake, achana naye. Kama akija kwako muda wa kula akawa anakula kama mwizi, ujue sio mlafi tu, ila hajiheshimu wala hakuheshimu. Mwanamke bora anatakiwa akushauri kutotumia pesa, muda vibaya.
Unamwambia mtu, "Aisee, mimi maharage siyapendi".. Anakujibu "Hujapata mpishi anayepika vizuri na akaweka na nazi" Sijui ni kwanini watu uwa wanapata ugumu kuelewa kwanini mtu hapendi kitu ambacho wao wanakipenda.
Sijajua ni uYanga wangu au ni roho mbaya yangu.. Ila sijapenda Simba kumsajili Sowah.. Lijamaa linajua sana
Movies ambazo Zombies wake walikua wanakichafua. Na sikujutia kuzicheki ni:- 1. Train to Busan (2016) 2. World War Z (2013)
Kuna muda, Ni bora kutomjali mwanamke wako, ata akikuacha unajua sababu.. Kuliko kumjali , alafu akikuacha uanze kujiuliza tatizo ni nini..
Kuna muda sio kwamba mpenzi wako amekuacha.. Ni Mungu ameamua kukuokoa..
Unaweza kuwapata wanawake mara nyingi tu. Ila wewe kujipata inaweza ikatokea mara moja tu..
Hakuna haja ya kwenda honeymoon nje ya nchi, au kwenda kwenye mahoteli makubwa makubwa.. Kama mke wako ndo anataka, basi umeingia sehemu sio sahihi. Anataka kujionyesha kwa watu tu, kwenu mbeya, nenda mbeya, kwenu ni shinyanga. Nendeni uko. Ni kuweka misingi kama mwanaume.
Ila watu 😁, Kwenye comment kuna jamaa kaandika. "Nimejaribu kuvaa viatu vya mrisho mpoto, ila nimekumbuka anatembeaga peku".
Watu hawajali. Kama una sehemu ya kulala au hauna. Kama watu wanakuheshimu au hawakuheshimu. Watu wengi ni wabinafsi. Wanaangalia maisha yao na matatizo yao wenyewe. Usitegemee mtu akutie moyo. Lazima upambane mwenyewe Kila kitu unapaswa kukifanya kwa juhudi zako mwenyewe.
Kwa maisha yanavyokuendea hivi sasa Bado unamchukia baba yako au sasa umeanza kumuelewa ?
Hakuna mwanaume anapenda kuwa na mwanamke kibonge.. Ukiona mwanaume anasifia wanawake vibonge au yuko na mahusiano na mwanamke kibonge. Hana hela.
Wewe kuwa mtu mwema, lakini usijisumbue kuthibitisha hilo kwa mtu yeyote..
Unamwambia Mwanamke, 'Unajua mimi nakupenda sana, unanifanya nakua na furaha.' Anajibu 'Vipi kuhusu mke wako sasa' Nikamjibu "Mke wangu yeye sasa hakupendi". Wanawake wanapenda sana ku focus na watu wasiowapenda kuliko watu wanaowapenda..
Wanawake wengi wa Kitanzania wako tayari kufa au kutekwa kuliko kumpa zawadi mwanaume wake. Wanaamini kuwa neno “zawadi” linatoka kwa mwanaume na kwenda kwa mwanamke. Kitu pekee wanachowapa wanaume ni kitumbua, kitu kilekile walichowapa washkaji zao wengine waliochana nao.
Kuna jamaa kaandaa party ya kumvalisha mdada pete ya uchumba, mdada hajatokea. Mwanamke kama haulizii ishu za ndoa lakini anafanya majukumu yote kama mke, usimuoe mwanamke wa aina hiyo. Anakuonea huruma, we unahisi unapendwa. Wanaume, jifunzeni ukatili kutoka kwa wanawake.
Kama umeoa, na mke wako hana mambo mengi.. Na wewe ukaamua kuacha mambo yote ya hovyo (kuchepuka) Kuna amani flani hivi utaipata na utulivu flani hivi kwenye maisha yako. Yawezekana hujui jinsi gani Mungu alivyokutendea Mema.
Kuna mshikaji ana watoto 6 wakiume, alivyopata mtoto wa 3, akasema ngoja nitafute ka binti. Kila akiwasha anatoka wakiume. Saizi wako 6.. Kasema haendelei tena.
Wanawake wenyewe wanajua kila wanapolala na mwanaume wasiyempenda, kuna sehemu ndani yao inayokufa kidogo, na wanakosa amani. Wanakubali kulala na mwanaume wasiyempenda ili wapate kitu cha kutimiza ndoto au tamaa zao binafsi. Ila ni kitu kinawaumizaga sana..