Ayubu Madenge
@ayubu_madenge
Dad|Friend|Citizen|Humble servant of the people
Raia wa Afrika Kusini mwenye asili ya India Ahmed Kathrada alisimamisha masomo ili afanye harakati za kupinga Ubaguzi. Yeye na Mandela ni miongoni mwa waliofungwa kisiwa cha Robben Island. Alikataa kuwa Waziri Serikali ya Mandela akasema “sikupambana ili nije kupewa nafasi”.

Jana ilikuwa Mandela Day, siku ya kumkumbuka kiongozi aliyejitoa ili atete HAKI na aliyepinga Ubaguzi. Mwaka 2019 miaka Sita iliyopita nilipata nafasi ya kuzungumza na vijana wenzangu juu ya namna tunavyoweza kumuenzi mzee Madiba. Sehemu ya mazungumzo hayo yapo kwenye video hii.
Captain Ibrahim Traoré aliingia madarakani baada ya kufanya mapinduzi 2022.Akaahidi kurejesha utawala wa Kidemokrasia mwaka 2024 na hivyo watu walipaswa kupiga kura. Lakini 2024 ilipofika akatangaza kusogeza mbele uchaguzi hadi mwaka 2029. Jana ametangaza kuifuta tume ya Uchaguzi

Kwa wote mnao wasaidia Wazazi au Walezi wenu ninawaombea mifuko yenu isikauke kamwe. Mikono yenu isikose riziki na mioyo yenu ipate amani kila wakati. Baraka za MUNGU ziwafuate kila muendako na milango ya fursa izidi kufunguka mbele yenu.
Kiongozi wa Burkina Faso, Captain Ibrahim Traore akionesha mfano kwa wananchi wake kwa kutoa damu yake ili ikasaidie kuokoa maisha ya watu. Traore aliwahimiza wananchi wake kujali na kulinda afya zao na kuwa tayari pia kuchangia damu ili kuwasaidia wenye uhitaji.

Caitlan Morgan alihitimu degree ya Finance and accounting chuo kikuu Swansea. Ameomba kazi mara 646 ndani ya miezi 18 ila hakufanikiwa kupata ajira. Sasa amepata ajira baada ya kuomba kazi kwa mara ya 647. Uingereza takwimu zinasema watu milioni 1.2 wanaomba nafasi za kazi 17000

Wataalam wa location haya majengo yako Mkoa gani hapa Tanzania na ni majengo ya nini?

Pesa huwa zinakata, marafiki wanabadilika, mipango inaharibika, umaarufu unaisha, connections zinakauka lakini MUNGU hajawahi kupungua. Mtegemee wakati wote, sio tu wakati wa Magumu yako bali pia wakati wa Mafanikio yako. Leo kabla ya kulala sema “MUNGU, mimi si kitu bila wewe”.
Ndani ya saa 48, Wakenya wamechanga Tsh Milioni 10 kwa ajili ya kumpa David Maraga kwa ajili ya kampeni za Urais kwenye uchaguzi wa mwaka 2027. Maraga ni Jaji mkuu mstaafu wa Kenya na itakumbukwa kuwa mwezi Mei alikuja Tanzania kusikiliza kesi ya Tundu Lissu.

Ukiona haya majengo unajua kuwa upo Chuo gani hapa Tanzania?

Waziri Mkuu wa Israel yaani Benjamin Netanyahu amekumbwa na changamoto ya afya iliyosababishwa na “food poisoning”. Sasa atapumzika kwa muda wa siku 3 wakati akipata matibabu na huku akiendelea na kazi zake taratibu. Taarifa imetolewa na ofisi yake. Netanyahu sasa ana miaka 75.

Zamani ukiwa mwanafunzi wa Elimu ya juu jamii na nchi ilikuwa inajivunia uwepo wako. Wanafunzi wa Elimu ya juu walikuwa wanaheshimika na kutegemewa katika kufanya tafiti na kushauri mambo kitaalamu. Walisimama katika UJUZI, UKWELI na HAKI na nchi ilinufaika sana na uwepo wao.
Mabasi 99 ya mwendokasi kwa ajili ya njia ya Mbagala yapo tayari na yanatarajia kufika hapa nchini ndani ya siku 21. Mpaka kufikia Agosti 15, Mabasi mengine 101 nayo yatakuwa yamefika nchini. Mradi huu utaanza Septemba 1 na utaendeshwa na Kampuni binafsi ya Kitanzania.

Takribani jezi 100,000 za Lamine Yamal zimeuzwa kote duniani ndani ya saa 24 baada ya kinda huyo kupewa jezi namba 10 ya Barcelona iliyowahi kuvaliwa na Lionel Messi na Ronaldinho. Mauzo ya jezi hizo yanakadiriwa kuwa sawa na Tsh Bilioni 41 ndani ya saa 24 tu.

Urefu wa futi 6.1 na uzito wa Kg 80, kijana wa Guinea mwenye uwezo mkubwa wa Soka hasa katika kupiga pasi na kukaba. Mchezaji mwenye sifa na uwezo wa kucheza mashindano ya Kombe la dunia ngazi ya Vilabu. Leo Eng Hersi amemleta 𝐌𝐎𝐔𝐒𝐒𝐀 𝐁𝐀𝐋𝐋𝐀 𝐂𝐎𝐍𝐓𝐄 kutoka CS Sfaxien

Captain Ibrahim Traoré ameifuta tume ya uchaguzi ya Burkina Faso na amesema kuwa uwepo wake ni matumizi mabaya ya Pesa. Hivyo chaguzi zitakuwa zinasimamiwa na Wizara ya mambo ya ndani. Pia amesema kuifuta tume hiyo kutasaidia chaguzi zao zisiwe zinaingiliwa na mataifa ya nje.

Kuna nyakati baraka za MUNGU zinafungua milango ya fursa na mafanikio ambayo Degree zako, ujuzi wako na Connections zako zote zisingeweze hata kutikisa milango hiyo. Daima endelea kumtegemea MUNGU, hata pale ambapo unaona jitihada zako zinatosha kukupa kile unachokitaka.
Hakuna picha inayo trend leo kama hii. Tabasamu la Freeman Mbowe linazungumza.

Mtengenezaji filamu mashuhuri wa India yaani S S Rajamouli anatajiria kurekodi filamu yake mpya hapa Tanzania mbugani Serengeti. Filamu hiyo itakayoitwa SSMB29 inasubiriwa kwa hamu na itahusisha waigizaji nguli akiwepo Priyanka Chopra. Bajeti ya Movie ni Tsh Bilioni 304
