TAMWA Zanzibar
@TAMWA_Zanzibar
TAMWA Zanzibar is a non-partisan not for profit sharing, non-Governmental professional membership organization. #MwanamkeNiKiongozi #ZuiaUkatiliZanzibar
Waandishi wa habari wanahitaji ulinzi wanapotekeleza majukumu yao hasa kipindi cha uchaguzi. Wao ni daraja la taarifa kwa jamii, hivyo kila mwandishi anapaswa kupewa haki sawa ya kupata taarifa, kupewa kitambulisho, na kuripoti bila bughudha wala vitisho. #UhuruWaHabariZanzibar @
TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na @unwomen UN na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam @udsmofficial (UDSM) wameandaa mafunzo maalum kwa waandishi wa habari 30 wa Zanzibar kuhusu namna ya kuripoti na kukemea ukatili dhidi ya wanawake katika kipindi cha uchaguzi. Mafunzo haya yanafanyika…




“Wamenisema sina pesa, wamenithibitishia jina langu likirudi nikawatie mikwaju mbele ya watoto zao, wengine wamesema watahama shehia", Asma Sadik. Haya ni baadhi ya maneno ya dharau anayokutana nayo Asma Sadik, mtia nia nafasi ya Uwakilishi kupitia CCM jimbo la Tunguu. Lakini…
Waandishi wa habari 10 kutoka vyombo mbalimbali kisiwani Pemba wameanza mafunzo ya uandishi wa habari zinazohusu wanawake, uongozi, na mabadiliko ya tabianchi. 📍 Mafunzo haya yanafanyika katika ofisi za TAMWA Zanzibar zilizopo Mkanjuni. 🌱 Lengo ni kuwawezesha wanahabari…



👨👩👧👦 Mwanaume anaposhiriki clinic, anajenga familia yenye afya na mshikamano! Afya ya uzazi si jukumu la mwanamke peke yake — ni safari ya wote wawili. Twende clinic pamoja, tuamue pamoja, tulinde afya pamoja. #srhr
Tunapoianza wiki mpya, tunawashukuru waandishi wote kwa kuendelea kuandika habari zinazojenga uelewa na kuhamasisha nafasi sawa kwa wanawake katika uongozi. Tunawashukuru kwa kuendelea kuwa sehemu ya mapambano ya haki na usawa. 👏🏽 Shukrani za pekee kwa @joelbert_ kwa…

📢 TAMWA-ZNZ inakaribisha maombi kwa Waandishi na Wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa kada ya habari kujiunga na mafunzo ya uandishi wa Habari za ujumuishi na haki za Watu Wenye Ulemavu! 📝 Jaza fomu ya maombi hapa: 👉 forms.gle/mX2RjpmELUVn1R… Mwisho wa kutuma maombi: 25 Julai 2025.

📊 “Je, utampigia kura mwanamke akigombea nafasi ya uongozi?” Hii ndiyo poll aliyoiendesha @Lubasha – mmoja wa content creators waliopitia mafunzo yetu kuhusu wanawake na uongozi. Matokeo? ➡️ 56% ya waliochangia walisema HAWATAMPIGIA KURA MWANAMKE. Hii si tu takwimu – ni…

✊🏽 Kutoka kwenye mafunzo hadi kwenye uwanja wa siasa! Maryam, kijana mwanamke jasiri, sasa ametia nia kugombea uwakilishi jimbo la Kiembe Samaki. Anasema: "siwezi kukatishwa tamaa, nitatimiza ndoto zangu" ✊🏽 From leadership training to the political arena! Maryam, a brave…
TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) wameandaa mkutano maalum na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pamoja na waandishi wa Habari kujadili umuhimu wa kupatikana kwa sheria rafiki ya habari visiwani Zanzibar. 📍…




🎭 "Wewe mwanamke utagombea nini? Kaa nyumbani!" Hii ndiyo sauti ambayo wanawake wengi huambiwa kila uchaguzi unapokaribia. Lakini kupitia @kidundotz mmoja wa content creators waliopitia mafunzo yetu ya wanawake na uongozi ameonesha jinsi elimu na uelewa unavyoweza kubadili…
Maneno yao yasikuzuie kutimiza ndoto zako.💪🏽👩🏽⚖️ Katika jamii zetu, bado kuna sauti zinazopunguza ujasiri wa wanawake wanaoamua kugombea nafasi za uongozi. Lakini mwanamke shupavu ni yule anayesimama imara licha ya maneno ya kukatisha tamaa. Tunamshukuru @joelbert_ kwa kuibua…

Wananchi wa Shehia ya Mfenesini, Mbuzini na Mwakaje wakishiriki mkutano wa jamii ulioandaliwa na TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na JUWAUZA kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuunga mkono ushiriki wa wanawake katika uongozi. 👥 Tukiwa pamoja, tunaweza kuijenga jamii yenye usawa na haki…




"Ili tujivunie kuwa tumepiga hatua katika uongozi wa wanawake, au tufahamu kama bado tunahitaji kuongeza juhudi, ni lazima tuwe na takwimu sahihi zinazothibitisha hali halisi." — Mohammed Khatib, Mtaalamu wa Ufuatiliaji na Tathmini, TAMWA ZNZ.

Leo tumejumuika na wadau mbalimbali kujadili zana maalum ya kufuatilia takwimu za uongozi kwa kuzingatia jinsia na watu wenye ulemavu (PwDs). 📊 Mkutano huu muhimu umeandaliwa na TAMWA ZNZ na washirika wa mradi wa SWIL ambao ni JUWAUZA na PEGAO kwa kushirikiana na Ofisi ya…




Leo tarehe 16 Juni, TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na Wadau wa utetezi wa haki za watoto Zanzibar inaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakiil, Kikwajuni Zanzibar. Lengo ni kujadili na kutathmini ustawi na maendeleo ya watoto hasa katika…



TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na JUWAUZA imeandaa mkutano wa siku mbili katika ofisi za TAMWA zilizopo Tunguu, ukihusisha asasi za kiraia, wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari, na wawakilishi kutoka vyama vya siasa. Lengo la mkutano huu ni kujadili kwa kina…




"Kwenye vyama vya siasa ni lazima tuwe makini na haya makundi ya hamasa tunayoyaanzisha, haya pia yanachochea sana udhalilishaji kwa vijana wetu", Bakar Hamad Mratibu wa Program LSF.

"Wanaume mtuache tupumue, mkiona wanawake wamesimama majimboni msiwatilie fitna kwa wanawake wenzao, mtuache tupige kampeni kwa amani na kushika nafasi za uongozi", Halima Omar, Afisa dawati chama cha CUF.

"Suala la usawa wa kijinsia bado liko chini katika vyama, wanaoendesha madawati ya kijinsia hawana elimu ya kutosha juu ya utekelezaji wa dawati hili, lazima tuyajenge haya madawati ndani ya vyama yawe na uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu yao ndani ya vyama", Bi Asha Aboud,…
