Martin Maranja Masese
@IAMartin_
MMM | Public Spirited | Sperm That Won The Race | Think Deep, Don’t Sink | Cogito, ergo Sum | Hasta la Victoria Siempre | Patria o Muerte, Venceremos |
Taifa ambalo redioni asubuhi hadi mchana wanajadili michezo. Mchana hadi jua linapozama wanajadili umbea. Jua likizama wanarudi kwenye michezo. Usiku wanajadili ngono hadi pakuche. Hakuna vipindi vya taaluma, ujasiriamali, kilimo, midahalo. Hilo ni TAIFA lipo kaburini kitambo.
Siasa za uchatu ndani ya CCM. Mwananchi kutoka Arusha anapiga nondo hapa. Msikilize. Utapata kitu. #NoReformsNoElection
CCM, MSAJILI wa VYAMA vya SIASA; WANACHEKESHA. Kuna jitihada zinazoendelea kufunika dosari kubwa za kikatiba, kikanuni, na kisiasa katika mchakato wa kumteua mgombea Urais CCM mwaka 2025. Mchakato huo ulikuwa na dosari za msingi na kimantiki. Wachambuzi na wapambe wa DOLA…


Waturutumbi ambao hawajawahi kukemea utekaji na mauaji ya raia hata kwa emoji tu ndiyo leo wanataka kutufundisha jinsi ya kumzodoa mtu kama Askofu Joe Gwajima ambaye amekemea utekaji na Balozi Polepole anayekosoa utaratibu wa upatikanaji wa mgombea Urais wa CCM. Tutamuunga mkono…
Unawasha VPN na kuingia 𝕏 ili kumwaga sifa na kuwapongeza watawala na kuikingia kifua Serikali iliyofungia mtandao wa 𝕏 ni upumbavu ambao haujawahi kutokea tangu uwepo wa Dunia.
Wote hatuwezi kuleta mageuzi kwa pamoja. Wengine watakuwa Kizimkazi, wengine BAR, wengine bizee na mamipira ya Kariakoo, wengine umbea, wengine ubwabwa na zambarau. Lakini wote watafurahia mageuzi yakipatikana. Umeamua kwa vyovyote kukataa MaCCM (Interahamwe), usichoke. Usiogope.
Mtu mmoja anatoa takwimu za uongo ndani ya mwezi mmoja. Halafu uso mkavu. Dingi haoni noma kabisa. Kwa hiyo baada ya mbogamboga kufunga zoezi la kuchukua fomu mkaendelea kutoa fomu nyingine uchochoroni? Au ni fomu za waganga wa kienyeji? Hivi anawaonaje MaCCM wenzake huyu kiumbe?


Binafsi, sikuingia CDM kwa sababu ya mtu na siwezi kuondoka CDM kwa sababu ya mtu… ni mtu mpumbavu pekee yake anaingia na kuondoka CDM kwa sababu ya mtu. Tuishi CDM kwa kufuata misingi ya uanzishwaji CDM, falsafa na itikadi zake. Hutoweza kuyumbishwa na hisia, tamaa na upepo…
Wafuasi wa ‘ubwabwa’ na ‘zambarau’ kwanini wamekereka sana na maneno mazito ya Humphrey Polepole? Walikwazika hivi pia kwa maneno ya Askofu Joe Gwajima. Je, hawataki wanachama wa CCM waishambulie Serikali ya CCM na chama chao? Hawataki kusikia mtu anakemea na kukataa utekaji?
Gaborone, Lusaka, Harare, Windhoek, Lilongwe, Nairobi, Johannesburg; huko unazunguka barabarani na mitaa hukutani na mabango ya kusifu kiongozi wa chama tawala au kiongozi wa Serikali. Huu utaratibu wa kumwaga sifa kwa watawala kupitia mabango kwetu tumerithi kutoka kwa nani?
Mtu wangu wa nguvu, @millardayo inawezekana jana ulichoka na kazi nzito ya kutujulisha kuhusu matukio yaliyojiri katika DIRA 2050. Ukiamka baada ya kupata supu ya ulimi hapo Palm Village, tujulishe habari za Balozi #HumphreyPolepole. Balozi ametema nyongo sana. Tackles shazii..


Namsikiliza Balozi #HumphreyPolepole hapa. Balozi anashambulia vizuri akitokea pembeni. Tackles hapa na pale. Anafinya. Anabaruza. Ni hakika mafunzo ya kuishi CUBA kama Balozi yamemsaidia sana. Let’s go!

Kumeshona. Hakuna nafasi. Mtu mmoja ashuke, nipande.


Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Sura ya 20), Kanuni za ulinzi wa mashahidi za mwaka 2025. Kanuni zimetengenezwa chini ya kifungu cha 188(3). Tangazo la Serikali Na. 430 la 11/07/2025. Kanuni hizi zimepitishwa na zimeanza kutumika. Katika kesi ya @TunduALissu watazitumia.


Kitu naamini, pamoja na mambo yote mabaya ambayo yanatokea, CHADEMA TUPO KATIKA NJIA SAHIHI na TUTAVUKA SALAMA. VITA ni kubwa sana kutoka kwenye DOLA na marafiki wa DOLA. Lakini, CHADEMA lazima ibaki salama na watoto wetu wataitumia kutengeneza TANZANIA nzuri na SALAMA waitakayo.
Dira ya Taifa au Dira ya CCM? Kama hakuna Katiba Mpya na bora, hiyo Dira ya Taifa ni kazi bure. Mafisadi wanaotajwa katika taarifa ya CAG wataendelea kutafuna mali za UMMA. Unaweza kutengeneza DIRA hadi 2050 lakini hutaki ‘electoral reforms’ kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa 2025?
Kuna viumbe ukiondoa maisha ya CHADEMA katika maisha yake, anabaki na nguo zake za ndani tu…. Wamepata hadhi na heshima wakiwa CHADEMA… wamekuwa wabunge, meya, madiwani kupitia CHADEMA… lakini ndiyo wametumika zaidi kuumiza taasisi, hisia za wanachama na wafuasi wa CHADEMA.
Yaani kuna watu wameumia kabisa Askofu Joe Gwajima kukemea utekaji? Kuna viumbe wamekwazika Ask. Joe Gwajima kuunga mkono hoja za NRNE? Hawa watu ni kwamba wanafurahia watu kutekwa na kuuwawa? Wanafurahi watu kuporwa haki ya kuchagua na kuchaguliwa? Au ndiyo watekaji wenyewe?
“Tuna uhuru wa kufikiri nje ya uwezo wa watawala wanavyofikiri. Na hakuna hata mtawala mmoja atakuja kunizuia na kunipangia namna ya kufikiri au aje kwako kukuzuia kufikiri” - Jenerali Twaha Ulimwengu
