Historia Yetu
@HistoriaYetu
Ukurasa kuhusu historia ya Tanzania. Kabla na baada ya uhuru. Tundikie 📧- [email protected]
Ndio maana yule Mama alilia sana. Mungu aendelee kumtia nguvu.

Usiku wa Jan 20, 1964, Mlinzi Mkuu wa Mwl. Nyerere Peter Bwimbo anapokea simu ya jaribio la mapinduzi ya kijeshi katika Kambi la Lugalo. Saa 2:30 Usiku Peter Mbwimbo katika Ikulu ya Magogoni Dar ew Salaam, anamgongea Mwalimu chumbani, anamtorosha kwa njia ya baharini kwa mtumbwi…

Sheikh Mohammad Idd amefariki leo Jan 30, 2025 katika Hospitali ya Mloganzila Dar es Salaam. Huyu ndio Shekhe wa kwanza Tanzania Bara kuwa na kipindi cha Televisheni.

📍📸China, 1960s Baada ya kuhudhuria mkutano Marekani kwa niaba ya Mwalimu Nyerere, Lucy Lameck na Bi. Titi waligeuza safari na kuelekea China bila idhini ya Mwalimu. Waliporejea nchini, wakiwa na zawadi za kumfurahisha Mwalimu, walijielekeza Msasani kuripoti kwake. Bi. Titi…

📍London, 1970s “Dunia nzima, tukio ambalo linakaribia kufanana zaidi na matendo ya Wajerumani kwa Wayahudi, ni makaburi wa Afrika Kusini dhidi ya Watu weusi.” Baba wa Taifa kwa kujiamini kwenye mahojiano haya alitamka wazi na kusema pia endapo Uingereza itaendelea kuigaia…
📍New Delhi, India, 1976 Waziri awasili India kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa India ndira Gandhi juu ya Amani ya Angola na mustakabali wake. 1975 baada ya Angola kupata Uhuru wake, iliingia katika vita mbaya ya wenyewe kwa wenyewe iliyohusisha makundi matatu; MPLA (ilisaidiwa…
Miezi mitano tu ya kufanya kazi kama Balozi wa Tanganyika UK, 1962 Balozi Christopher Kasanga Tumbo (Pichani) alijitoa TANU na kurejea nchini, kisha kuanzisha chama chake cha siasa cha People’s Democraric Party (PDP). Mwalimu hakupenda, akamuweka (Kizuizini) ‘House arrest’ kwa…

📍Kenya, Embakasi 1977 Ujumbe wa majirani Kenya kwa Mwalimu, hii ni baada ya Tanzania kufunga anga lake kwa ndege zote za Kenya kutua Tanzania kufuatia kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya miaka 10 (1967 - 1977). #TanzaniaVsKenya

📍Kampala, Chuo Kikuu Makerere April 1965 Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Rais Julius Nyerere wa Tanzania, akimtunuku Rais Jomo Kenyatta wa Kenya shahada ya heshima ya Udaktari wa Sheria. Na bila shaka, huo ndio wakati pekee ambapo Mzee alionekana akiwa amepiga goti.…

HEKAYA FUPI YA BOSI WA BENKI YA CRDB, ABDULMAGID NSEKELA Miaka 25 iliyopita, Abdulmajid Nsekela alikuwa kijana anayepokea cheti cha mafunzo ya huduma za bima kutoka kwa Dkt. Charles Kimei, aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB wakati huo. Leo hii, historia imejigeuza—Nsekela…

Chadema ilizaliwa 28/5/1992, hii list nzima aliye active leo kwenye chama ni Mbowe tu.
